Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Export Processing Zones Authority

Export Processing Zones Authority

News

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara atembelea Viwanda


SERIKALI yawahakikishia wawekezaji mazingira bora ya ufanyaji biashara katika kutumia fursa ya masoko ya ndani na nje ya nchi likiwemo soko la SADC, AGOA, AfCFTA na EAC.

Hayo yamesemwa tarehe 26 Mei, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo Nje (EPZA) na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb,) alipokutana na kuzungumza na meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeza nguo cha Tanzania Tooku Garment Company Limited kilichopo ndani ya eneo la mamlaka hiyo Ubungo External, jijini Dar es salaam.

Dkt. Kijaji amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara hivyo kupitia wizara yake ataendelea kuwafuata wawekezaji na kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ili shughuli za uzalishaji zisikwame.

kiwanda hiki cha Tanzania Toouk Garments ni cha mfano wa kuigwa kwani kimesaidia ajira, fedha za kigeni na kodi kwa serikali hivyo hatuna budi kukilinda na kutatua changamoto zinazowakabili Amesema Dkt. Kijaji.

Akizungumza katika ziara hiyo Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji Dkt. Tausi M. Kida amesema kuwa jitihada za haraka zinaenda kufanyika kutatua changamoto zinazomkabili mwekezaji huyo na kwa kushirikiana na wizara na taasisi nyingine kutatua changamoto za sera na sheria mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo Nje (EPZA) Bw. Charles Itembe amesema kuwa kiwanda cha Tooku Garment kimeajiri wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4,000) ambapo bidhaa zake huuzwa katika soko la AGOA.

Naye meneja mkuu wa kiwanda cha Tooku Garment Bw. Borja Trenor Casanova ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuboresha mazingira ya Uwekezaji hasa kwa kuwatembelea wawekezaji na kutatua changamoto mbalimbali.